RCC DAR YAPITISHA BILIONI 992 MWAKA WA FEDHA 2026/2027
Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) ikiongozwa na Albert Chalamila imepitisha kiasi cha shilingi bilioni 992.6 ikiwa ni rasimu ya bajeti kwa ajili ya shughuli za miradi ya maendeleo ya jamii pamoja na mishahara ya watumishi wa Mkoa huo kwa mwaka wa fedha 2026/2027
Akizungumza katika Mkutano wa kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam RCC uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashairi ya Manispaa ya Temeke RC Chalamila amesema kamati hiyo imependekeza fedha hizo kutokana na uhitaji wa Mkoa huo ambao ni taswira ya nchi katika nyanja anuai ikiwemo uchumi na diplomasia
Pamoja na mapendekezo hayo ya bajeti RC Chalamila amezungumzia kikao cha bodi ya barabara ya Mkoa huo ambacho kimefanyika kabla ya mkutano wa kamati ya ushauri ya mkoa huo ambacho kimezitaka TARURA na TANROAD kuharakisha mchakato wa kuzisajili barabara ambazo hazipo kwenye mtandao wao ili ziingie kwenye mpango wa bajeti ujao huku akisisitiza kazi hiyo ifanyike kwa mfumo wa kijimbo ndani ya wiki moja huku pia akihimiza suala la uwepo wa mfuko wa barabara "Road Fund"
Aidha kupitia mkutano huo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amezungumzia changamoto ya msongamano wa magari kwenye jiji hilo ambapo amesema ni muhimu kuwa na mchanganuo mzuri wa aina ya magari na yapite kwenye barabara zipi kwa kuzingatia mahitaji kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi zingine huku akitolea mfano wa suala la mabasi kuingia mjini kiwa hakuna ulazima huo na amewataka viongozi kusimamia wakandarasi kukamilisha ujenzi wa miradi ya barabara kwa wakati.
Aidha amezungumzia changamoto ya wamiliki wa malori kutokuwa na maeneo ya kuegesha magari na badala yake wamekuwa wakipaki kwenye maeneo ya hifadhi za barabara.
Post a Comment