WAFANYABIASHARA MKOANI MTWARA WAHIMIZWA KUTOA USHIRIKIANO KWA TRA
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya amewataka Wafanyabiashara mkoani hapo kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika katika zoezi la utoaji elimu ya kodi ikiwemo kulipa kodi kwa wakati.
Rai hiyo ameitoa wakati alipofanya mazungumzo na maafisa wa TRA waliomtembelea ofisini kwake leo tarehe 9 Machi, 2026 kwa ajili ya kuanza Kampeni ya utoaji wa elimu ya kodi mlango kwa mlango.
“Rai yangu naweza kusema kwamba, maendeleo yote tunayoyaona kama vile, barabara, maji, elimu, afya, miradi mbalimbali inayoendelea haya yote yanarejeshwa kwetu kwa kulipa kodi, niwasihi wana Mtwara kuwapa ushirikiano maafisa wa TRA wanaopita kuwapa elimu ya kodi”, alisema Mhe. Mwaipaya.
Ameongeza kuwa, Maafisa wa TRA hawapiti madukani kwa ajili ya kufunga maduka, bali wanapita kuwaelimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi, kutatua kero za walipakodi na kupokea maoni mbalimbalim hivyo watoe ushirikiano kwa ajili ya kuwezesha zoezi
Post a Comment