WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UMWAGILIAJI BONDE LA EYASI
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 6, 2026 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika Bonde la Eyasi, lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.
Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji utagharimu shilingi bilioni 38.4. Hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba mwaka huu.
Kukamilika kwa mradi huo utanufaisha zaidi ya wakulima 2,500 kutoka skimu za Mang’ola Barazani, Maleckchand, Laghangareri, Mbuga Nyekundu, Jobaji na Dumbechand, zenye zaidi ya hekta 5,000.
Aidha, utekelezaji wa mradi huo utasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa upotevu wa maji unaotokea katika mifereji ya asili, hatua itakayoongeza ufanisi wa matumizi ya maji na kuimarisha uzalishaji wa mazao katika eneo hilo.

Post a Comment