ILALA WAMALIZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026


Mwenge wa Uhuru 2026,  umemaliza mbio zake katika wilaya ya Ilala, ikiwa ni wilaya ya kwanza kuanza mbio hizo katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo katika Wilaya ya Ilala miradi 7 yenye thamani 52,088,900,245.72 imepitishwa na Mwenge wa Uhuru na  hakuna mradi uliokataliwa.


Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika miradi ya mwenge , Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa  Wazo Mwang'onda, amewaeleza wananchi malengo ya mwenge wa uhuru ni kuleta matumaini, kumulika ndani na nje ya mipaka yetu, kuleta amani, matumaini na upendo.


Jambo linaloendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kama ilivyokua na kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Nyerere .


Mbio za  Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, katika wilaya ya Ilala, chini ya Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo,   umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kitega uchumi cha DDC Kariakoo, ujenzi wa barabara ya lami mtaa wa Lindi, ujenzi wa kisima cha Ilala kota, ujenzi wa kituo cha afya Mchikichini, ujenzi wa shule mpya ya sekondari kitunda relini, ujenzi wa kituo cha polisi Bonyokwa na Kikundi cha vijana Fighter wanaojishugulisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki.  


Mwenge wa Uhuru 2026  April 14,  unaendelea Wilaya Kigamboni ambapo utatembelea, utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.


Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026 inasema Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo





No comments