KINGU AITAKA SERIKALI KUDHIBITI MATUMIZI MENGINE ILI KUPUNGUZA MFUMO WA BEI WA MAFUTA



Mbunge wa Ikungi Magharibi (CCM), Elibariki Kingu ametoa ushauri kwa Serikali ya nini kinapaswa kufanywa kwa sasa ili kupata ahueni ya ongezeko la bei ya mafuta inayopendelea kuwaumiza wananchi.


Kingu amesema hayo leo Jumatano, Aprili 8, 2026 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2026/2027, ya Sh12.5 triloni bugeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo amesema Serikali inapaswa kuchukua hatua za dharura kukabili ongezeko la bei ya mafuta ikiwemo kupunguza vikao: “Waziri Mkuu, mkienda kufanya hili, mtaona nchi inafurahi.”

Aprili mosi, 2026, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ilitangaza ongezeko hilo la bei za mafuta, linaloelezwa kuchochewa na mgogoro wa kimataifa unaoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, ulioanza Februari 28, 2026.

No comments