SERIKALI YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT. SAMIA KUMEGA SEHEMU YA ENEO LA SHAMBA LA MITI SHUME
Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kumega eneo la shamba la miti la Shume lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga kwa ajili ya shughuli za kijamii za Wananchi
Akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Abdallah aliyetaka kufahamu hatua za utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ya kuwapatia wakazi wa kata za Lukozi, Shume na Manolo sehemu ya eneo la shamba hilo, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde(Mb) kwa niaba ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema kwa sasa Serikali iko katika hatua za uchambuzi wa maombi yakiyowasilishwa na vijiji, kata na Halmashauri hiyo.
“Serikali inatambua ahadi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia uwezekano wa kupata ardhi kidogo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii.” Amesema Mhe. Silinde
Post a Comment