TANZANIA NA BENKI YA DUNIA WAKUTANA KUPITIA MIRADI IDA-21
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha ngazi ya Wataalamu na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, ambacho kilijadili miradi ya kipaumbele ya Serikali katika sekta mbalimbali itayoombewa ufadhili Benki ya Dunia kupitia Mzunguko wa 21 wa IDA (IDA-21 Cycle),
Kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayoendelea jijini Washington DC, Marekani.
Aidha kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Sosthenes Kewe, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Benki hiyo.










Post a Comment