WAZIRI KOMBO AKUTANA NA BALOZI WA DENMARK, WAAZIMIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jesper Kammersgaard, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark.
Mazungumzo hayo yamefanyika Aprili 27, 2026, katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali za maendeleo, zikiwemo uwekezaji, afya na kilimo.
Aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia na kupanua wigo wa ushirikiano katika sekta za kimkakati kwa manufaa ya mataifa yote mawili.
Post a Comment