CCM KUENDELEA KUWAJENGA VIJANA KIITIKADI NA KIUONGOZI
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuthamini na kutoa kipaumbele maalum kwa vijana kwa kuwa ndio nguvu kazi ya chama na taifa kwa ujumla.
Dkt. Dimwa ameyasema hayo katika hafla ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) “DK. MWINYI UVCCM USHINDI PARTY” iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mafunzo na Uongozi UVCCM Dambwe, Tunguu Zanzibar.
Amesema CCM itaendelea kuwaandaa vijana kiitikadi, kiuongozi na kiutendaji ili wawe viongozi bora wa sasa na baadae wenye uwezo wa kusimamia na kulinda maslahi ya chama.
Aidha, Dkt. Dimwa amewahimiza vijana kuwa wazalendo, wachapakazi na wabunifu kwa kutumia fursa za teknolojia kujiajiri pamoja na kuchangia maendeleo ya taifa.
Katika hatua nyingine, amesema CCM itaendelea kuwaamini vijana kwa kuwapa nafasi mbalimbali za elimu na mafunzo ya amali ili wawe vijana walioiva katika fani mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa chama na taifa.




Post a Comment