DAR CITY SASA MGUU SAWA KUIKABILI PETRO ATLÉTICO DE LUANDA
Timu ya kikapu ya Dar City imekamilisha mazoezi yake ya mwisho jijini Kigali nchini Rwanda, ikiwa tayari kabisa kwa mchezo wa Play-Off wa Mashindano ya Basketball Africa League dhidi ya wapinzani wao, Petro Atlético de Luanda. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo, tarehe 23 Mei 2027, majira ya saa 1:00 usiku.
Mashindano ya BAL yanaendelea kuwa jukwaa muhimu kwa timu za Afrika kuonyesha vipaji na ubora wa mchezo wa kikapu, na mchezo wa leo kati ya Dar City na Petro Atlético unatarajiwa kuwa miongoni mwa michezo inayovutia zaidi kwa wapenzi wa kikapu barani Afrika.
Dar City sasa inaingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi, hatua ambayo itaiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo na kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano makubwa ya kikapu barani Afrika.







Post a Comment