DKT. KIJAJI: NJOONI MSHUHUDIE VIVUTIO VYA UTALII KATIKA BANDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII BUNGENI
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameakikwa kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika viwanja vya Bunge kushuhudia vivutio na kazi mbalimbali za uhifadhi na utalii zinazofanywa na wizara hiyo
Mwaliko huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea na kukagua Banda la Wizara hiyo kwa lengo la kuhamasisha Utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania
’’Leo ilikuwa ni siku yetu kubwa, siku ya maliasili na utalii ambapo tumewasilisha hotuba ya Bajeti yetu kwa ajili ya mwaka 2026/27 lakini tumeleta na utekelezaji wa yale ambayo tumeahidi kwa mwaka 2025/26. Lakini hatujaishia hapo tumewaletea na Banda la amaonesho ili wabunge washuhudie yale ambayo tulikuwa tukiwaeleza katika hotuba ya bajeti ili waone yale ambayo tumetekeleza kwa mfano’’ Amesema Dkt. Kijaji
Dkt Kijaji amesema katika maonesho hayo fursa ya kushudia vivutio mbalimbali vya utalii kwa vitendo ikiwemo kuona kwa uhalisia namna ambavyo watalii wameongezeka nchini
‘’Ukienda kwenye Banda la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wamekuja na kifugaa kinachoonesha vivutio mbalimbali vya Utalii lakini ukifika kwenye Banda la Ngorongoro unaweza kushuhudia vivutio vya Utalii Mubashara" alibainisha Dkt. Kijaji
Aidha, Dkt. Kijaji amesema maonesho hayo ni hatua muhimu ya kuunga kazi na Juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuakisi namna ambavyo vivutio hivyo vimeongeza Idadi ya Watalii nchi ambapo kwa mwaka huu idadi hiyo imeongezeka maradufu
Dkt. Kijaji aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Katibu Mkuu Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Nkoba Mabula Manejimenti ya Wizara pamoja na Watumishi na Maafisa wa Uhifadhi.






Post a Comment