DKT. YONAZI AUPONGEZA UBALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, amepongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Dkt. Yonazi ametoa pongezi hizo alipotembelea ubalozi huo akiwa katika ziara ya kubadilishana uzoefu kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga inayofanyika Maputo kuanzia Mei 25 hadi 29, 2026.
Amesema watumishi wa ubalozi wanafanya kazi nzuri ya kuiwakilisha Tanzania na kuendeleza diplomasia ya uchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji.
Kwa upande wake, Mwambata Fedha wa ubalozi huo, Bw. Samson Marwa, alimshukuru Dkt. Yonazi kwa ziara hiyo na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kihistoria kati ya Tanzania na Msumbiji.






Post a Comment