RAIS SAMIA AIPA TANZANITE MILIONI 50 BAADA YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya shilingi milioni 50 kwa timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20, “Tanzanite”, kufuatia mafanikio yao ya kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la wanawake nchini Tanzania.


Akizungumza leo Mei 20, 2026 jijini Dodoma wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima ya timu hiyo, Makonda amesema hatua hiyo ya Rais ni sehemu ya kuthamini na kuhamasisha juhudi za wachezaji hao walioandika historia kubwa kwa taifa.


Hafla hiyo pia imehudhuriwa na nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand, ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.


Timu ya “Tanzanite” imeandika historia kwa kuwa timu ya kwanza ya wanawake kutoka Tanzania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

No comments