ZIPIGIENI KURA HIFADHI ZETU ZA TAIFA: MSIGWA
Watanzania wametakiwa kupigia kura vivutio vya utalii hapa nchini vilivyoingia kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo za Kimataifa za Utalii Duniani ( World Travel Awards 2026), ili ziibuke kidedea ikiwemo Hifadhi ya Taifa Kitulo na Pori la akiba la Mpanga-Kipengele.
Wito huo umetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa, Mkoani Njombe, mbale ya Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini, alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali iliyoangazia mambo ya maendeleo yaliyofanywa katika Mikoa ya nyanda za juu Kusini.
Bw. Msigwa alisema kuwa, Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanya kazi kubwa ya maboresho ya miundombinu katika vivutio vya utalii nchini vikiwemo vilivyopo Mikoa ya Nyanda za juu Kusini jambo linalopelekea kuvutia watalii wengi wa nje na wandani kutembelea maeneo hayo.
Amesema kuwa, kura nyingi zikatazo wezesha vivutio hivyo vishinde itasaidia kuvitangaza zaidi ulimwenguni na kuvutia watalii hali itakayo saidia kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Tanzania imefanya vizuri mwaka huu kwa kupata jumla ya uteuzi ( nominations) zaidi ya 85 katika vipengele 41 kwenye tuzo za "World Travel Awards (WTA) 2026".
Katika kipengele kikubwa na maarufu cha "Vivutio Bora vya Utalii Afrika (Africa's Leading Tourist Attraction 2026)", Tanzania imetawala kwa kuingiza vivutio saba (7) kati ya 14 vilivyoteuliwa barani kote.

Post a Comment