MAKAMU WA RAIS KUWA MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 kitakachofanyika Juni 5 jijini Dodoma, akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa kutembelea mabanda ya maonesho kuelekea kilele cha maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, amesema utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila sekta na si la taasisi chache pekee.
Amesema sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, usafiri na mawasiliano zinapaswa kuzingatia kanuni za uhifadhi wa mazingira ili kuchangia maendeleo endelevu na kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Masauni amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za mazingira pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo, akieleza kuwa ni fursa ya kujifunza na kujadili mikakati ya pamoja ya kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.















Post a Comment