MBAPPÉ AWAANDIKIA MASHABIKI WA UFARANSA UJUMBE WA SHUKRANI
Nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé, leo ameandika ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wa nchi hiyo, akiwashukuru kwa sapoti waliyoitoa kwa timu katika kipindi chote cha michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Mbappé ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa Ufaransa, ikiwa ni takribani wiki moja baada ya timu hiyo kuondolewa katika hatua ya nusu fainali na Hispania kwa kufungwa mabao 2-0.
Katika ujumbe wake, nyota huyo wa Real Madrid amesema timu ya Ufaransa haikuwapa mashabiki mwisho waliokuwa wakiutarajia, huku akieleza kuwa kushindwa kutwaa ubingwa huo ni jambo linaloumiza.
Hata hivyo, Mbappé amesema anajivunia juhudi zilizofanywa na kikosi hicho katika mashindano hayo, huku akiwashukuru mashabiki kwa kuendelea kuwaunga mkono hata katika nyakati ngumu.
Mbappé pia amewashukuru wachezaji wenzake kwa mchango wao, akieleza kuwa mafanikio yake binafsi katika mashindano hayo, ikiwemo kufunga mabao mengi, yasingewezekana bila kazi ya pamoja ya timu.
Mshambuliaji huyo amesema ingawa Kombe la Dunia limekwisha, bado safari ya timu ya Ufaransa inaendelea, akisisitiza kuwa kutakuwa na michezo mingine na fursa nyingine za kuendelea kuwakutanisha mashabiki na timu yao ya Taifa.

.jpg)

Post a Comment