REAL MADRID YAWEKA MKONO KWA WINGA WA IVORY COAST YAN DIOMANDE



Klabu ya Real Madrid ya Hispania imefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili winga wa kimataifa wa Ivory Coast, Yan Diomande, kutoka klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani.

Diomande, ambaye alionyesha kiwango kizuri katika Kombe la Dunia la FIFA 2026, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji vijana waliovutia vilabu vikubwa barani Ulaya.

Taarifa zinaeleza kuwa Real Madrid inatarajiwa kulipa zaidi ya Euro milioni 100 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo, huku baadhi ya ripoti zikikadiria thamani ya jumla ya dili hilo kufikia takribani Euro milioni 135.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuongeza kasi, uwezo wa kupambana na mabeki mmoja kwa mmoja pamoja na nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Real Madrid.

Diomande, ambaye ana umri wa miaka 19, amekuwa akiwindwa na baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya, lakini Real Madrid imeonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kukamilisha usajili wake.

Iwapo dili hilo litakamilika, Diomande atakuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi kusajiliwa na Real Madrid katika dirisha hili la usajili, huku klabu hiyo ikiendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya.

No comments