MILIONI 432 KUJENGA KITUO CHA TAALUMA EDWARD MPOGOLO DAR ES SALAAM.

 


HALIMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam, imetenga kiasi cha shilingi milioni 432,  kujenga kituo cha  umahili wa  taalumu  kitakachofahamika kwa jina Edward Jonas Mpogolo Center for Excellence Capacity  Building.


  Hayo yameelezwa katika hafla ya utangazaji matokeo ya mitihani ya ndani na utoaji wa tuzo kwa wanafunzi na  shule za sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo kwa kidato cha kwanza cha pil cha tatu na cha sita, jiji Dar es Salaam.


Aidha tuzo hizo zikitolewa kwa  shule za sekondari zilizofanya vibaya  kwa kukabidhiwa vinyago maalumu vya mpingo.


Akikabidhi tuzo hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema, mkakati uliopo katika kuboresha sekta ya elimu ni kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.


"Pia kutekeleza maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuboresha miumdombinu ya elimu na ubora wa elimu itakayo mwezesha mhitimu kupata taaluma yenye tija," alisema Mpogolo.


Amesisitiza, Jiji la Dar es Salaam, linaendelea na ujenzi wa sekondari za ghorofa  zenye vifaa vya kisasa,vitabu, kuimarisha nidhamu na uwajibikaji, matumizi ya teknolojia  na kutekeleza mkakati wa kufuta ufaulu wa daraja sifuri na la nne.


Alipongeza halimashauri ya jiji hil kuamua kuwa na kituo cha taaluma alichosema  kitakuwa ni chachu ya kuongeza ufaulu, kuwaongezea ujuzi walimu na kufanya tathimini ya elimu.







No comments