KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YAPOKEA TAARIFA YA WIZARA HIYO

 


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenye kiti wake Mhe. Timotheo Mnzava, Leo Agosti 17, 2026 Bungeni Jijini Dodoma imepokea taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu migogoro ya mipaka katika maeneo yaliyohifadhiwa na hatua za utatuzi wa migogoro hiyo pamoja na taarifa ya hali ya sekta ya wanyamapori nchini ikiwemo mafanikio, changamoto na hatua za utatuzi wa changamoto hizo.


Katika uwasilishaji wa taarifa hizo Kamati ya Kudumu ya Bunge imeisisitiza Wizara kuhakikisha inatatua migogoro ya mipaka iliyopo kwa wakati na kwa kuzingatia utu kwa wananchi vilevile kuhakikisha kila mtu anapatiwa haki yake bila uonevu ili kuendana na kauli ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya 'Kazi na Utu'.


Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameihakikiahia Kamati hiyo kuwa Wizara ipo kazini kutatua migogoro yote inayojitikeza katika mipaka ya maeneo yaliyohifadhiwa na kuwa Wizara itasimamia misingi ya utu katika kila hatua ya utatuzi wa migogoro hiyo.


















No comments