ATUHUMIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MKEWE KWA WIVU WA KIMAPENZI.
JESHI la polisi mkoani Rukwa linamshikilia Maiko Sosolo Kazikulima (35) mkazi wa Kijiji Cha Mashete kata ya Mashete wilayani Nkasi mkoan Rukwa kwa tuhuma za kumuua mkewe Victoria Mputa (32) kwa kumpiga kichwani akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa Rukwa SACP Shadrack Masija amesema tukio hilo limetokea Jana J,Nne September 8,2026 majira ya saa 3 usiku wakati wakitoka kilabuni pamoja, ndipo ulipozuka ugomvi miongoni mwao uliohusishwa na wivu wa kimapenzi na kusababisha kuuawa kwa mwanamke huyo.
Amefafanua kuwa mtuhumiwa ambaye alikua mume wa marehemu wakiwa njiani kabla hawajafika nyumbani mzozo mkubwa kati Yao uliibuka huku Mume akiendelea kumtuhumu mkewe kwa kuwa na mahusiano mengine na Wanaume wengine kiasi Cha kuchukua maamuzi ya kuanza kumpiga na rungu kichwani kinyume Cha Sheria.
Kamanda Masija amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Polisi na kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Sambamba na hilo amewataka Wananchi kuendelea Kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwabaini wahalifu na kuwa katika kipindi hiki wamekua wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Wananchi kitu kilichopelekea wahalifu wengi kunaswa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Post a Comment