AFISA TARAFA KATERERO NA WATAALAMU WA KISHERIA WA MAMA SAMIA WATATUA MIGOGORO YA WANANCHI KATA YA KAIBANJA.
Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku akiongozana na Wataalamu wa Kisheria wa Mama Samia (MSLAC) chini ya Ndugu Selemani Selemani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wamefika Kata ya Kaibanja kusikiliza migogoro ya wananchi na kuitatua.
Ajenda namba moja kwenye Tarafa ya Katerero ni kusikiliza kero za wananchi na kuitatua lengo likiwa kuifanya jamii kuishi kwa amani na upendo isiyo na migogoro.
Afisa Tarafa Bwanku na Timu ya Wataalamu wa Kisheria wa Mama Samia kutoka Halmashauri ya Bukoba waliita pande zote zinazolumbana kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kaibanja na kusikiliza hoja za kila upande na baadae kutoa suluhu ya migogoro yote bila upendeleo huku elimu ya masuala ya kisheria ilitolewa pia.






Post a Comment