WAZAZI TUWEKEZE KATIKA ELIMU KWA WATOTO SIO KUWACHEZA NGOMA - KIKWAYU
Jamii wilayani Kisarawe , Mkoani Pwani imetakiwa kubadilika na kuwekeza katika elimu kwa watoto ili kuhakikisha wanafanya vizuri shuleni.
Wito huo umetolewa wilayani Kisarawe, Na mdau wa masuala ya elimu na michezo Saidi Kikwayu katika kata Vikumburu kwenye mahafari ya kidato cha nne shule ya sekondari vikumburu wakati anazungumza na wazazi, walimu na wanafunzi.
Kikwayu amesema ni wakati wa jamii ya Kizaramo kufuta imani ya kushindwa kuwekeza katika masomo kama zinavyowekezwa shughuli ili kuondoa mawazo hasi juu ya jamii hiyo nchini.
Amebainisha kuwa endapo jamii itabadilika kuanzia nyumbani wazazi na walimu kushirikiana ni rahisi kujua maendeleo ya mtoto shuleni kuliko kuacha jukumu ilo kwa walimu pekee jambo linalokosa nguvu upande mmoja.
Ameongeza kuwa ili wanafunzi wafanye vizuri shuleni kunahitajika ufatiliaji wa mtoto katika masomo, nidhamu na kupenda kusoma bila kushurutishwa kwa njia yoyote licha ya changamoto ambazo serikali inaendelea kuzitatua kwa nyakati mbalimbali.
Amesema, fursa ya elimu bila malipo inayotolewa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inapaswa kutumiwa vema kwa kila mtoto anayeanza shule elimu ya msingi na kuendelea na sekondari amalize elimu hiyo.
Akijibu risara iliyosomwa na wanafunzi wa kidato cha nne katika mahafari ya 11 shuleni hapo kwa wahitimu 57 wanaotarajiwa kufanya mitihani yao ya kuhitimu mwaka huu, Kikwayu amewapongeza walimu na wazazi waliotoa ushirikiano hadi sasa.
Kwani katika risara hiyo, wanafunzi hao wameomba kusaidiwa upatikanaji wa Maji safi na salama, vifaa vya maabara, ujenzi wa bweni ili kuwapunguzia mwendo wanafunzi wanaotoka mbali, na kuomba vifaa vya computa viongezwe shuleni.
Jambo ambalo limeungwa mkono na risala iliyotolewa na Mkuu wa shule hiyo ya sekondari Pacience Mponda alipozungumzia mafanikio ya miaka 3 nyuma ya ufaulu kwa shule hiyo unatokana na juhudi za walimu na wanafunzi, mitihani ya kujipima ya ujirani mwema, na mpango mkakati wa wanafunzi kupata chakula shuleni jambo lilifanya kuanzisha shamba ili walime na kupata chakula.
Aidha ameebainisha, umuhimu wa uwepo wa bweni shuleni hapo utasaidia wanafunzi kupata muda wa kujisomea, kupunguza mimba za utotoni na utoro kwa wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kufika shuleni.
Ombi ambalo, mgeni rasmi katika mahafari hayo ya 11 shuleni hapo Saidi Kikwayu amelipokea kwa kuchangia mifuko 50 ya sementi ili kuanza chagizo la upatikanaji ufumbuzi wa bweni kwa wanafunzi.
.jpeg)

.jpeg)



Post a Comment