SERIKALI YAWEKEZA BILIONI 8.4 KUBORESHA UFANISI KWA MAMLAKA YA UFUNDI STADI (VETA)



Serikali ya Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa wa shilingi bilioni 8.4 kwa Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini (VETA), ikiwa ni hatua ya kuboresha ufanisi na kuongeza ujuzi katika taasisi hiyo muhimu kwa maendeleo ya ufundi nchini. 

Hayo yamesemwa Leo Jiji Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, wakati akikabidhi vifaa vya kisasa kwa baadhi ya taasisi zilizo chini ya VETA.

Profesa Nombo ameeleza kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza ubora wa elimu ya ufundi stadi na kusaidia vijana kupata ujuzi wa vitendo utakaowasaidia katika soko la ajira.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya VETA, taasisi za serikali, na sekta ya kibinafsi ili kukuza sekta ya ufundi stadi na kuongeza fursa za ajira.

Profesa Nombo a amesema kuwa kupitia ushirikiano na taasisi mbalimbali za serikali na benki, VETA imeweza kuingiza vijana waliokuwa wakifanya kazi katika sekta isiyo rasmi katika mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi ambapo inasaidia vijana kuwa na ujuzi wa kisasa, na kwa upande mwingine, inatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.

Hata Hivyo Profesa Nombo amewaomba waajiri na viwanda kushirikiana na VETA na taasisi nyingine za serikali ili kutoa mafunzo zaidi kwa vijana huku Akisisitiza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuleta mapinduzi makubwa katika ufundi stadi na kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania.





No comments