ZAIDI YA VITUO NANE KUTUO HUDUMA YA UPASUAJI HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM


Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya ndania katika sekta ya afya ndani ya kipindi cha miaka mitatu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Mpogolo ameyasema wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya afya inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.

Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi, hususan katika ngazi za kata na mitaa. 

 Mpogolo, amebainisha kuwa Serikali inatambua umuhimu wa sekta ya afya, ndiyo maana tunahakikisha miradi yote ya afya inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati.

Aidha, Mpogolo ametoa wito kwa wakandarasi wazawa wenye uwezo kuchangamkia fursa za miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, huku akiwaonya wale “janja janja” wasio na uwezo wasithubutu kuomba kazi hizo, kwani Serikali haitavumilia uzembe wala ubadhirifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa Halmashauri itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya  ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa, na kuleta manufaa kwa wananchi.

Katika ziara ya leo, Mkuu wa Wilaya ametembelea Kituo cha Afya cha Mchikichini, pamoja na Kituo cha Afya cha Mzinga.

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya ndani ya Wilaya ya Ilala.





No comments