BANDARI YA MTWARA NA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKIANA KATIKA USAFIRISHAJI KOROSHO GHAFI
Bandari
ya Mtwara imekusudia kushirikiana na sekta binafsi kuendesha Bandari Kavu lengo
likiwa ni kufungasha kontena za Korosho ghafi zinazosafirishwa kupitia Bandari
hiyo.
Meneja
wa Bandari hiyo, Ferdinand Nyathi, amesema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ya kukagua maeneo, shughuli na vifaa kwa
ajili ya kuhudumia mizigo ya korosho kupitia Bandari ya Mtwara kwa msimu wa
Korosho wa mwaka 2025/2026.
Mpango
huo wa kushirikiana na sekta binafsi za Bandari ni kuhakikisha ufanisi mkubwa
katika kuhudumia mzigo wa korosho.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Sawala, amesema lengo la uamuzi huo ni kuwahakikisha
ufanisi wafanyabiashara na wasafirishaji kusafirisha mizigo yao kwa urahisi na
kuendelea kutekelezwa agizo la serikali la kusafirisha korosho kupitia Bandari
ya Mtwara.

Post a Comment