MBUNGE WA ILALA MUSSA AZZAN ZUNGU AUKAMATA USPIKA WA BUNGE LA TANZANIA
Mbunge wa Ilala kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mussa Zungu, amechaguliwa kwa kura 378 kuwa Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
Zungu, amewashinda wagombea wenzake Watano kutoka vyama mbalimbali vya siasa katika uchaguzi uliosimamiwa na Mwenyekiti, Wiliam Lukuvi
Akitangaza matokeo hayo leo Bungeni jijini Dodoma, Katibu wa Bunge, Baraka Leornad, amesema jumla ya Wabunge 383 wamepiga kura, huku kura tatu zikiharibika, na wagombea wawili kupata kura moja kila mmoja.
Vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo ni NRA, DP, AAFP, NLD, na ADC.
Zungu anakuwa Spika wa Nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo limeshaongozwa pia na Maspika wanawake akiwemo Anne Makinda na Dokta Tulia Ackson.
Wabunge watamchagua Naibu Spika wa Bunge, ambapo Chama Cha Mapinduzi kimempitisha Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Sillo, kuwa mgombea wa nafasi hiyo.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Spika wa Bunge, Zungu, ameahidi kuliongoza Bunge kwa haki, uwazi na ushirikiano, akizingatia Katiba, Sheria, na Kanuni za Kudumu za Bunge, bila upendeleo.

.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)

Post a Comment