BUGURUNI VIZIWI WASHINDA VIA CREATIVE KITAIFA 2025


SHULE ya Msingi ya Viziwi Buguruni imeibuka mshindi wa kwanza kitaifa katika mpango wa VIA Creative 2025, unaoendeshwa na Kampuni ya TotalEnergies kwa lengo la kuhamasisha elimu ya usalama barabarani kupitia ubunifu na sanaa kwa wanafunzi.


Washindi hao wametangazwa Novemba 13, 2025 jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, ambapo Shule ya Sekondari Ndalala na Shule ya Msingi Ubungo NHC ziliibuka washindi wa pili na wa tatu.


Kupitia ushindi huo, Shule ya Msingi ya Viziwi Buguruni itaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ngazi ya kanda yatakayofanyika Novemba 26, 2025, na ikiwa itafanya vizuri, itapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa jijini Paris, Ufaransa.


TotalEnergies pia imeahidi kutekeleza mapendekezo ya wanafunzi wa shule hiyo kwa kuweka alama za barabarani zinazoonyesha uwepo wa shule ya viziwi katika eneo la Buguruni ili kuongeza usalama.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania, Bw. Mamadou Ngom, amewapongeza wanafunzi kwa ubunifu na dhamira yao ya kuimarisha usalama barabarani.












No comments