RAIS SAMIA ATUMIA SAA 1:44 KUWAAPISHA MAWAZIRI 27 NA MANAIBU WAZIRI 29

 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,amewaapisha mawaziri 27 na manaibu waziri 29 aliowateua Novemba 17,2025 kuunda Baraza la Mawaziri kwa Muhula wa Pili wa  Serikali ya Awamu ya Sita.


Rais Samia amewaapisha viongozi hao Novemba 18,2025,Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma,hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.



Viongozi hao wamekula kiapo cha uaminifu na kiapo cha maadili ya viongozi wa Umma kilichosimamiwa na Kamishna wa Maadili,Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi shughuli iliyoanza 05:12 asubuhi na kukamilika saa 06:56 mchana.


Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba,Spika wa Bunge Mussa Azzan na Jaji Mkuu wa Tanzania George Masaju.


Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Asha-Rose Migiro,Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira,Maziri Wakuu Wastaafu Kassim Majaliwa na Mizengo Pinda







No comments