DKT. HOMERA ASISITIZA AMANI SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, ametoa rai wa wananchi kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa amani na utulivu. 


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, ameyasema hayo wakati akiwatakia Watanzania wote na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kote nchini, heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2026. “Nawaombea mwaka huu uwe wa mafanikio makubwa, tija, na neema tele.”


Pia Mheshimiwa Waziri anawasihi wananchi wote kusherehekea kwa amani, upendo, na utulivu na kusisiza umuhimu wa kudumisha mshikamano kama Taifa huku wakifurahia baraka za msimu huu wa sikukuu na wapendwa wao.


Waziri Mh. Dkt. Homera amewakumbusha wananchi wote kutekeleza wajibu wa kusherehekea kwa kuwajibika, kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za nchi, kufurahia kwa usalama, kulinda amani na kujiandaa kwa mwaka mpya wenye mafanikio zaidi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

 

No comments