MRADI WA BILIONI 2.3 KUKUZA UCHUMI MKOA WA PWANI


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amekutana na uongozi wa TPDC ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mussa Makame, kujadili utekelezaji wa mradi wa bomba la gesi la Kinyerezi–Chalinze. Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuufanya Mkoa wa Pwani kuwa kitovu cha kimkakati kiuchumi.


Mradi huu unatarajiwa kuchochea uwekezaji mkubwa, hususan katika sekta ya viwanda, hali itakayoongeza uzalishaji na kukuza mapato ya mkoa. Mhe. Kunenge amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Mkoa wa Pwani na TPDC ili kufanikisha azma hiyo ya kukuza uchumi wa viwanda.


Kwa upande wake, TPDC imethibitisha kuwa upembuzi yakinifu umekamilika, ambapo mradi utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.3. Mradi huo utatekelezwa na makandarasi wa Gulf Interstate Engineering na Paulsam Geo-Engineering Co. Ltd, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 15 tangu kusainiwa kwa mkataba.

No comments