MSIGWA: TUWE WALIMU WA MATUMIZI BORA YA NISHATI SAFI KWA JAMII
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewataka Watumishi wa wizara hiyo kuwa mabalozi wa matumizi bora ya nishati safi ya kupikia baada ya mafunzo waliyoyapata kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Msigwa amesema hayo, Desemba 11, 2025 wakati akizungumza na watumishi hao Mtumba jijini Dodoma, ambapo amewataka kuwa mfano kwa jamii ili ijifunze faida za matumizi bora ya nishati safi.
"Sisi ni binadamu, na tunatumia nishati majumbani, tujue matumizi sahihi ili kuepuka kusababisha madhara, ukipata mafunzo haya unafundisha na wanaokuzunguka kwenye jamii ili elimu ifikie wengi zaidi" alisema Msigwa.
Vilevile, ametumia nafasi hiyo kuhamasisha watumishi wa Serikali kujenga utaratibu wa kusoma vitabu ili kuweza kuongeza maarifa na kutoa huduma bora kwasababu kusoma vitabu kunasaidia kujifunza zaidi.
Katika mafunzo hayo watumishi walipata elimu kuhusu elimu ya afya na Usalama mahali pa kazi, Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF), matumizi ya nishati safi majumbani na umuhimu wa kujiwekea utaratibu wa kusoma vitabu.

Post a Comment