SHUGHULI ZA KIBINADAMU BONDE LA MTO RUVU YATAJWA KUPUNGUZA UZALISHAJI MAJI, DAWSCO WAELEZA

Uzalishaji wa maji umepungua kutoka uzalishaji wa lita milioni 534.6 kwa siku hadi kufikia lita milioni 270, ambazo ni sawa na upufungu wa lita milioni 264.6 kwa siku.

Hata hivyo pamoja na upungufu huo imeeelzwa kwa hali ilivyo sasa hivi Mtambo wa Ruvu Chini iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku hivi sasa unazalisha maji lita milioni 50 kwa siku, huku Mtambo wa Ruvu Juu wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 196,  sasa uzalishaji wake umepungua na kufikia lita milioni 150.

Hii ni kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam-DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire.
Alikuwa akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania-TEF.

Mhandisi Bwire ametoa sababu za kupungua kwa uzalishaji maji na hivyo kusababisha changamoto ya uhaba wa maji katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Sababu za uhaba wa upatikanaji wa maji ni Mvua za masika zilinyesha chini ya wastani mwezi Machi -Mei, 2025
“Kuchelewa kwa mua za Vuli zilizotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba - Desemba, 2025 na Mto Ruvu kuacha njia yake ya asili kwenye eneo la Kitomondo na kutengeneza mchepuko.

“Sababu nyingine ni kuongezeka kwa Joto kutoka nyuzi joto 29-31C hadi nyuzi joto 33.2-34.2 (TMA), hali hii imesababisha kina cha maji kupungua kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maji kupotea kwa njia ya Mvuke.

Aidha, sababu nyingine ni kuongezeka  kwa shughuli za kibanadamu (kilimo, ufugaji) ndani
ya Bonde la Mto Ruvu.
Hata hivyo wakati hatua mbalimbali za muda mfupi zikiendelea kuchukua kukabiliana na hali hiyo Bwire amesema DAWASA inawaomba wananchi kuwa wahimilivu katika
kipindi hiki cha mpito na kuhifadhi maji yanayopatikana

Pia DAWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Pwani, Bodi ya Bonde la Wami-Ruvu, inaendelea kufanya doria kwenye eneo la Mto Ruvu kuhakikisha hakuna matumizi mengine ya maji kutoka kwenye mto.

Hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuyagawa na kuyasimamia maji kidogo yanayoendelea kuzalishwa kwa uwiano sawa, kudhibiti mivujo ya maji kwa wakati ili kuhakikisha maji kidogo yanayopatikana yaweze kuwafikia wateja pamoja na kutoa elimu ya kuhifadhi maji na matumizi bora ya maji katika kipindi hiki 

Wakati hatua zinachukuliwa za mrefu ni kuanza kwa utekelezaji wa Gridi ya maji ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kutoa maji Mto Rufiji kuja Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Lindi pamoja na kuongeza uchimbaji wa visima vya uzalishaji maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Mkoa wa Dar es salaam.

No comments