SIMBA YAGEUKIA LIGI KUU YASHUKA NA MKAKATI MZITO DHIDI YA MBEYA CITY KOCHA MATOLA KUIONGOZA KESHO
Kocha wa wekundu wa msimbazi Simba Selemani Matola amesema maandalizi yamekamilika kuelekea katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambapo nia ni kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo
Matola amekiri kuwa mchezo huo kwao ni muhimu na hautakuwa rahisi kwao kupata ushindi lakini watakata kupambana na kupata matokeo ya ushindi.
"kwa sasa hatuangalii michezo ya kimataifa ile imeshapita lakini kwa sasa tunaangalia mchezo uliokuwa mbele yetu."
"katika mchezo huo kila timu inakuja ikiwa na lengo la ushindi hivyo huu ni mchezo mwingine na tutarajie kuwa tutakuja na mbinu na mkakati mpya katika mchezo ili matokeo ya ushindi yabaki upande wetu"
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji David Kameta "Duchu" amesema wao tayari wamefanya maandalizi na wana hari kubwa katika mchezo huo watapata matokeo ya ushindi.

Post a Comment