KITUO CHA UBIA CHAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, ameanza kutekeleza maagizo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Katika utekelezaji huo, Kafulila, amekutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii siku moja baada ya Rais Samia kutangaza, wakati wa uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050 uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, kuwa nchi sasa inaingia katika hatua ya utekelezaji wa vitendo na kwamba muda wa maneno umekwisha.
“Ili kufikia lengo la kujenga uchumi utakaokuwa na uzalishaji wa bidhaa na huduma wenye thamani ya Dola za Marekani trilioni moja katika miaka 25 ijayo (2026–2050), lazima kuwe na mshikamano wa dhati kati ya serikali, sekta binafsi, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla,” alisema Kafulila katika kikao hicho.
Rais Dkt Samia alisema
"Sekta binafsi imepewa takribani asilimia 70 katika utekelezaji wa Dira hii kwa miaka 25 ijayo," alisema.
Nyenzo nne zilizozinduliwa kusaidia utekelezaji wa Dira 2050 ni: Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV), Mwongozo wa Taifa wa Ufuatiliaji na Tathmini, pamoja na Mkakati wa Mawasiliano.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment