SIMBACHAWENE ATAKA MIFUMO YA MAGEREZA IBADILISHWE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema kuna haja ya kubadili mfumo wa Magereza nchini ili kuendana na kasi ya dunia huku akigusia dhamira ya serikali kupitia baadhi ya sheria na kuzifanyia mabadiliko ili kuweza kuboresha masuala ya Haki Jinai.


Ametoa kauli hiyo  leo jijini Dodeoma baada ya kuapishwa kuwa  Mwenyekiti wa Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji  sambamba na wajumbe wengine wawili.


Naye Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma Mheshimiwa, Dkt. Juliana Masabo amepongeza juhudi zinazoendelea katika kutoa haki kwa watuhumiwa hali inayopelekea tatizo la uchelewaji wa upelelezi kupungua.

No comments