TANZANIA KUIMARISHA UHUSIANO NA MAREKANI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo anafanya ziara rasmi ya kikazi jijini Washington DC nchini Marekani.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania Washington DC, katika ziara yake hiyo Waziri Kombo atakutana na wadau mbalimbali muhimu katika kuimarisha uhusiano wa baina ya Tanzania na Marekani.
Akiwa nchini Marekani, Waziri pamoja na masuala mengine atakutana pia na kufanya mazungumzo ya kina na Serikali na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani.
Miongoni mwa viongozi ambao tayari amekutana nao ni Mbunge machachari wa Chama cha Republican- Brian J. Mast wa Jimbo la Florida ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani na kukubaliana mambo kadhaa juu ya uimarishaji wa uhusiano huo na Tanzania pamoja na kupokea mwaliko wa kamati yake kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.

Post a Comment