BUNGE LA TANZANIA NA MOROCCO LAFANYA VIKAO

Ujumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, umefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Maendeleo ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco, Mhe. Zaina Chaimi.


Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Zaina Chaimi amesema kuwa sekta ya kilimo ni miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi wa Morocco, akibainisha kuwa nchi hiyo ni mzalishaji mkubwa wa mbolea duniani, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa mapato ya taifa hilo.


Katika hatua nyingine, ujumbe wa Bunge la Tanzania pia umekutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa Fedha za Serikali, Mhe. Mohamed El-Hejira, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kibunge katika masuala ya usimamizi wa fedha za umma, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya Tanzania na Morocco.

No comments