TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA ALGERIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Mhe. Ahmed Attaf Jijini Cairo nchini Misri.


Mazungumzo hayo yamefanyika  tarehe 19 Desemba, 2025 pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje  wa Afrika na Urusi 

uliofanyika jijini Cairo, nchini Misri.


Katika kikao hicho, Mawaziri hao wamekubaliana  kushirikiana kwenye masuala ya nishati, uwekezaji, pamoja na  kuimairisha sekta ya utalii na kuanzisha safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Algeria. 


 Pamoja na hayo, Mhe. Waziri  Kombo amewakaribisha wawekezaji kutoka Algeria kuja kuwekeza nchini Tanzania kwenye sekta ya kilimo, ujenzi wa  viwanda  vya madawa,  pamoja na kuanzisha tume ya pamoja ya masuala itakayosimiamia masuala ya  uchumi  baina ya nchi hizo mbili.


Katika kikao Viongozi wengine waliohudhuria ni Mhe. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na  Michezo, Balozi Ali Bujiku, na Balozi Noel Kaganda.

No comments