TANZANIA NA INDIA ZAINGIA MAKUBALIANO TIBA ZA ASILI



Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa akisaini Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Afya Tanzania  na Wizara ya Afya India. Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Tiba Asili ikiwemo maeneo ya tafiti, mafunzo na kubadilishana uzoefu katika masuala ya Tiba Asili, sambamba na Mkakati wa WHO wa Tiba Asili 2025-2034. 

Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika New Delhi, India tarehe 19 Desemba 2025. India ni moja ya nchi iliyopiga maendeleo makubwa katika Sekta ya Tiba Asili.

No comments