SIMBACHAWENE AKAGUA MASHAMBA YA MAGEREZA KAGERA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.George Simbachawene(Mb),  Disemba 20, 2025 ametembelea Gereza Kitengule na kukagua shamba mkakati la kujitosheleza kwa chakula Magereza Mkoa Kagera  pamoja na kuongea na maafisa na askari wa Gereza Kitengule. 


Akikagua shamba hilo Mh.Simbachawene  amesema Jeshi la Magereza linahitaji kuboresha mfumo wa uzalishaji  mashambani  kwa kutumia vifaa vya kisasa kwenye kilimo na kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuepukana na changamoto ya hali ya hewa ambayo imekua ikiathiri uzalishaji  kila mara.


"Ili kumrekebisha Mfungwa kwenye nyanja  ya kilimo  anapoingia Gerezani  inahitajika mfungwa ajifunze kilimo cha kisasa  kwa manufaa ya Jeshi pamoja na maisha yake baada ya kumaliza kifungo chake" alisema Simbachawene


Pamoja na hayo Mhe. Simbachawene aliongea na wafungwa na mahabusu wa Gereza Kitengule  na kuwatia moyo kuwa  gerezani siyo mahala pa mateso wala pakuondoa utu wao,  bali ni sehemu ya kuwahifadhi  na kuwarekebisha  ili wanapomaliza kutumikia vifungo vyao wakawe raia bora na kuonesha yale waliyo jifunza wakiwa gerezani kwenye jamii.

No comments