WASANII KUIMBA KWENYE KAMPENI ZA CCM NI AJIRA YAO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amewashangaa wanaharakati wanao hamasisha chuki baina ya wasanii na wananchi, akisema kuwa wasanii kuimba kwenye kampeni za CCM ni ajira yao.
Mwigulu amesema hayo leo Desemba 17, 2025 wakati akizungumza na wakazi wa eneo la Tunduma mkoani Songwe ambapo yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua uharibifu wa miundombinu ya umma na mali binafsi zilizoharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.
Mhe. Mwigulu amesema, hizo ni chuki za kijinga zinapandikizwa na wanaharakati ambao wapo huko nje ya Nchi wamepewa hifadhi, akieleza kuwa wasanii hutumia vipaji vyao kujipatia kipato ikiwa ni Sehemu ya ajira yao.
"Ni nani aliyewaambia msanii akiimba kwenye kampeni basi yeye ni CCM?, ni chuki tu zakijinga, Serikali inahangaika kuhakikisha Vijana wanapata ajira, Sasa mtu anatumia kipaji chake alichopewa na Mungu kujipatia kipato watu wanachukia " aliongeza Dkt. Mwigulu
Ikumbukwe kuwa Wananchi wametilia mgomo kusapoti kazi za wasanii kufuatia madai kuwa wasanii hawasimami na jamii inapotokea shida Bali wao husimama Sehemu ya Serikali, jambo ambalo Wananchi wanaona ni usaliti.

Post a Comment