TANESCO KUENDELEZA JITIHADA UZALISHAJI WA UMEME

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Plasduce Mbossa, ameahidi shirika hilo kuendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji wa umeme ili kukidhi ongezeko la mahitaji nchini.


Mbossa amesema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Rhimo Nyansaho, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.


Mbossa amebainisha kuwa Dkt. Nyansaho ameiacha TANESCO katika mwelekeo mzuri wa kiutendaji.


Kwa upande wake, Dkt. Nyansaho amewashukuru wajumbe wa Bodi, na menejimenti ya TANESCO kwa ushirikiano katika kipindi cha uongozi wake.

No comments