CP KAVIRONDO AFANYA ZIARA ZA KIKAZI MKOA WA KAGERA AKAGUA MIFUGO, MASHAMBA NA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA


Kamishna wa Huduma za Urekebu Jeshi la Magereza, CP Amina Kavirondo,  afanya ziara ya kikazi mkoani Kagera, na kutembelea Gereza Rwamrumba, Kambi ya Mwisa, Gereza la Kilimo na Mifugo Kitengule pamoja na Gereza Rusumo.


Katika ziara hiyo, CP Kavirondo alikagua mashamba, mifugo na ujenzi wa jengo la utawala unaoendelea Gereza la Rusumo, huku akisisitiza umuhimu wa kilimo chenye tija na ufugaji bora ili kuongeza uzalishaji na kujitosheleza kwa chakula.

Aidha, aliwataka Maafisa na Askari kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali kwa kushirikiana na wataalam, pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni na miongozo ya Jeshi.

Pamoja na mambo mengine, CP. Kavirondo aliongea na Wafungwa wa Gereza Rusumo, huku akiwatia moyo kutumia kipindi chao cha kifungo kama fursa ya kujifunza na kujirekebisha, akisisitiza kuwa gereza ni sehemu ya urekebishaji.





No comments