WANANCHI WA KIJIJI CHA LAJA KARATU WAIPA KONGOLE TASAF



Wananchi wa kijiji cha Laja Wilayani Karatu Mkoani Arusha wameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya jamii -TASAF kwa miradi waliyoitekeleza katika kijiji hicho.

Wananchi hao wamezungumza hao kijijini hapo mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf pamoja na baadhi ya watumishi wa mfuko huo.

Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitamba kwa jina la Christina Lucas amesema Tasaf kupitia mradi wa Opec imefanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Laja pamoja na ujenzi wa madaraja katika kijiji hicho.



Amesema Ujenzi wa Shule hiyo ya Sekondari Laja pamoja na mabweni  umesaidia sana kuamsha ari ya elimu katika kijiji hicho.

Ameongeza kuwa awali wananfunzi katika kijiji hicho walilazimika kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule hali ambayo ilisababisha baadhi ya wanafunzi kutohudhuria masomo vema kutokana na adha hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Shadrack Mziray amewataka wananchi wa kijiji hicho kutunza miundombinu hiyo kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.



No comments