TRA YAHITIMISHA KIKAO CHA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI

Kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa nusu mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika kwa muda wa wiki moja kimehitimishwa leo tarehe 09.01.2026 jijini Arusha na kuja na mikakati mbalimbali ya kuzuia ukwepaji kodi na kuongeza wigo wa kodi. 

Akifunga kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC Kamishna Mkuu wa TRA Bw.  Yusuph Juma Mwenda amesema TRA itaendelea kupambana na wakwepaji wa kodi kwa njia mbalimbali ikiwemo kuimarisha mipaka, kuzuia magendo na kuwa na mbinu mbalimbali.

Amesema lengo la TRA ni kuongeza wigo wa kodi kwa kusajili biashara mpya na kuwasajili wafanyabiashara ambao bado hawajaingia katika mifumo ya kulipa kodi. 
"Haturidhiki na idadi ya walipakodi tulionao ikilinganishwa na idadi ya watanzania hivyo kazi iliyopo mbele yetu ni kwenda kuongeza wigo wa kodi" amesema Bw. Mwenda. 

Amesema wataendeza uadilifu kama ilivyo jadi ya TRA sambamba na utoaji wa elimu ya Kodi, kuwasikiliza walipakodi, kuwezesha biashara zao na kutatua changamoto zinazowakabili walipakodi" amesema Bw. Mwenda.

"Natamani siku moja TRA nisaidie nchi yetu kujitegemea" amesema Bw.  Mwenda.

No comments