USHIRIKISHWAJI WA JAMII NI NGUZO MUHIMU YA UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA BAHARI

 


Ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa mazingira, hususan rasilimali za bahari, umetajwa kuwa nguzo muhimu ya maendeleo endelevu, hususan katika kukuza uchumi wa buluu unaolenga kunufaisha wananchi moja kwa moja.


Katika kutekeleza azma hiyo, Shirika la WATONET limezindua mradi wa Uimarishaji wa Vikundi Shirikishi vya Usimamizi wa Rasilimali za Bahari na Pwani (BMU na VLC), utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2026 hadi 2028.



Akizindua mradi huo , Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, amewataka watekelezaji wa mradi huo kujikita zaidi katika utendaji unaolenga kuleta mabadiliko chanya kwa jamii badala ya kuendeshwa na siasa, ambazo zimekuwa zikikumba baadhi ya vikundi hivyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WATONET, Ndugu Liberatus Mokoki, ametoa wito kwa viongozi wa Serikali, taasisi, wadau wa maendeleo na wananchi kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha Kisiwa cha Mafia kinakuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza katika uhifadhi wa rasilimali za bahari nchini.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Ndugu Mussa Kitungi, amesema utekelezaji wa mradi huo unaakisi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kujenga uchumi jumuishi unaogusa maisha ya kila mwananchi.


Mradi huo unafadhiliwa na Blue Ventures na unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la WATONET, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia na Hifadhi ya Bahari Mafia (MIMP).




No comments