BMT YAKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO MKOA WA SHINYANGA KUJADILI MAENDELEO YA MICHEZO


Kikao kati ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Michezo ya Mkoa wa Shinyanga kimefanyika leo, Februari 16, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Mkoa Ndugu CP Salum Hamduni.

Kikao hicho kinalenga kuwakumbusha Wajumbe wa Kamati ya michezo majukumu yao ya msingi katika kusimamia na kuendeleza michezo, sambamba na kujadiliana kwa kina kuhusu hali ya maendeleo ya michezo katika mkoa huo.

Aidha, pande zote mbili zilibadilishana mawazo kuhusu mikakati ya kuboresha utendaji, kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha michezo inakuwa chachu ya maendeleo kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Ziara na vikao vya aina hii ni sehemu ya juhudi za BMT kuhakikisha Kamati za Michezo za Mikoa zinafanya kazi kwa ufanisi na kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

No comments