GAMOND AMEPEWA MIAKA MIWILI KUINOA STARS,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ametangaza kuwa Kocha Miguel Gamondi amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars).
Makonda ametoa taarifa hiyo leo Februari 16, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Gamondi amepewa mkataba huo kutokana na kuonesha uwezo mkubwa katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika Morocco, ambapo aliiongoza Taifa Stars kufika hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania akiwa kocha wa muda.
Serikali imeamua kumwajiri rasmi Gamondi ili aendelee kuijenga timu hiyo kuelekea AFCON 2027, mashindano ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji, ikiwa na lengo la kuwania ubingwa.
Post a Comment