MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA NI ALAMA YA UWEZO WA TANZANIA KUTUMIA RASILIMALI ZAKE ZA NDANI

 


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT) ni alama ya ukomavu na kielelezo cha uwezo wa Tanzania katika kupanga, kuamua na kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha na wataalamu wa ndani.


Ameeleza kuwa, ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayotoa kipaumbele na heshima kubwa katika shughuli za ulinzi, jambo linaloimarisha usalama na utulivu wa nchi.


Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Februari 24, 2026, wakati wa uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT) lililopo Kikombo, mkoani Dodoma.


Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa uzuri wa majengo hayo usiwe tu fahari ya Taifa, bali yaendane na matumizi yake halisi kwa kuimarisha na kusimamia ulinzi wa nchi, sambamba na kuendana na mikakati ya kisasa ya ulinzi kulingana na mahitaji ya wakati uliopo.

No comments