TANZANIA KUCHOTA UZOEFU KWA QATAR MAANDALIZI YA MICHUANO YA AFCON2027
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Paul Makonda amekutana na Balozi wa Qatar ndhini Tanzania na kufanya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Qatar
Makonda ametoa shukrani za Serikali kwa uhusiano imara uliopo kati ya mataifa hayo mawili, akisisitiza kuwa ushirikiano huo umeendelea kuzaa matokeo chanya katika sekta za maendeleo, uwekezaji na diplomasia ya kimkakati.
Katika mazungumzo hayo, Waziri aliwasilisha rasmi maandalizi ya Tanzania kuelekea kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, akibainisha fursa za uwekezaji katika miundombinu ya hoteli jijini Arusha, uboreshaji wa viwanja vya mpira wa miguu, pamoja na kukuza sekta ya utalii.

Makonda alisisitiza umuhimu wa kunufaika na uzoefu wa Qatar uliopatikana wakati wa kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2022, tukio lililotambulika kimataifa kwa ubora wa miundombinu, usimamizi na mchango wake mkubwa katika uchumi na maendeleo ya sekta ya michezo.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar alithibitisha dhamira ya kuendeleza ushirikiano huo kupitia kubadilishana uzoefu, kuimarisha ziara za kikazi, na kufuatilia mapendekezo yaliyowasilishwa kwa hatua za utekelezaji.

Pande zote mbili zilikubaliana kuharakisha mchakato wa makubaliano rasmi na kuendeleza miradi ya pamoja itakayochochea maendeleo ya michezo, utamaduni, utalii na uwekezaji, hatua inayotarajiwa kuongeza thamani ya kimkakati na kiuchumi kwa mataifa yote mawili.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment